16 Juni 2025 - 16:32
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu ya Ukaribu baina ya  Madhehebu za Kiislamu: "Uhalifu wa Israel ni Jeraha kwenye Mwili wa Umma wa Kiislamu"

Hojjatul Islam Wal-Muslimeen Dakta Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu ya Ukaribu baina ya Madhehebu za Kiislamu ameandika katika ujumbe wake kwenye Twitter yake kuwa: "Uhalifu wa Israel sio tu kuishambulia Iran, bali pia ni jeraha kwenye mwili wa Umma wa Kiislamu."

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kwa mujibu wa Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jumuiya ya Ulimwengu ya Ukaribu baina ya Madhehebu ya Kiislamu, maandiko ya ujumbe wa Katibu Mkuu ni kama ifuatavyo:

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu ya Ukaribu baina ya  Madhehebu za Kiislamu: "Uhalifu wa Israel ni Jeraha kwenye Mwili wa Umma wa Kiislamu"

"Kwa kuishambulia ardhi ya Iran na kumwaga damu zisizo na hatia za watoto wa ardhi hii, utawala katili wa Kizayuni umeongeza ukurasa mwingine katika kitabu chake cha aibu.
Jinai hii sio tu ni shambulio dhidi ya Iran bali pia ni jeraha katika mwili wa Umma wa Kiislamu.
Damu ya mashahidi wetu haitabaki bila kujibiwa;
Ahadi ya kimungu iko karibu".

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha